WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR ASISITIZA KUTUMIA MFUMO MPYA WA TEKNOLOJIA ILI KUWEZA KUHIFADHI VIZURI KUMBUKUMBU ZA DAWA ZANZIBAR

Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akitoa hotuba katika  mkutano wa kusaidia kazi zinazohusiana na Dawa na Vifaa Tiba kwa Serikali ya Zanzibar na Global Helth Supply Chain hafla iliofanyika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.

Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohammed amesema kuwa huduma za dawa zinazonunuliwa na Serikali pamoja zinazotolewa na wafadhili zinahitaji usimamizi mzuri  ili zisipotee kiholela.

Hayo aliyasema katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Zanzibar wakati akizungumza na Mkurugenzi Mkaazi wa mradi wa Global Health Supply Chain Program (LMU) Maver Tokai ambao unasaidia ugawaji na usambazaji wa dawa kwa Serikali katika vituo vya afya vya Zanzibar na Tanzania Bara .

Alisema kuwa ipo haja kuwepo kwa usimamizi mzuri wa dawa hizo ili kuona wafadhili wanapotoa  misaada inatumika kwa lengo lilokusudiwa la kuwapatia wananchi huduma bora za matibabu  .

Aidha alisema kuwepo kwa mfumo maalum ambao utaweza  kurahisisha kuhifadhi kumbukumbu katika komputa kutasaidia kudhibiti upoteaji wa dawa pamoja na kiwango cha dawa kilichopo zikiwemo na huduma za dawa zilizotolewa na ambazo tayari zimeshapita muda wa kutumika

 “Mfumo wa Tehama utasaidia  kwa kiasi kikubwa  kujua dawa zilizotumika ,zilizopo pamoja na zile ambazo zimeshamaliza muda ili kuweza kuzizuwia zisitumike kwa matumizi ya binaadamu “alisema Waziri huyo”.

Mkurugenzi Mkazi wa Global Helth Supply Chain Mavere Tukai akizungumza katika mkutano wa kusaidia kazi zinazohusiana na Dawa na Vifaa Tiba kwa Serikali ya Zanzibar na Global Helth Supply Chain hafla iliofanyika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.

Nae Mkurugenzi Mkaazi wa Mradi wa Global Health Supply Chain Program (LMU) Maver Tokai ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mashirikiano katika matumizi ya huduma za ugawaji na usambazaji wa dawa ambao unasaidia wananchi kupata matibabu.

Aidha alisema kuwa mradi wa ugawaji na usambazaji wa dawa umeanza katika mwaka 2016 hadi june 2021 ambao unatarajia kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma zilizobora.

Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dk Jamala Taib akisisitiza jambo alipotoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni rasmi katika mkutano wa kusaidia kazi zinazohusiana na Dawa na Vifaa Tiba kwa Serikali ya Zanzibar na Global Helth Supply Chain hafla iliofanyika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.

Nae Mkurugenzi Mkuu  Wizara ya Afya Zanzibar  Dk Jamala Talib amefahamisha changamoto zinazojitokeza katika ukaguzi wa mwenendo mzima wa dawa na utumiaji wa dawa kuna baadhi ya wafanyakazi kutokuwa waaminifu katika matumizi ya dawa.

Alifahamisha wafanyakazi ambao wamekosa uwaminifu kutokana na tamaa ya kujipatia pesa kwa haraka bila ya kujali azma ya Serikali kwa wananchi wake ya kuhakikisha wanawapatia wananchi wake huduma ya matibabu bure

Loading