SHIRIKA LA UTOAJI MIWANI LA SWEDEN WATOA HUDUMA ZA MACHO KITUO CHA AFYA PAJE

Katibu Tawala Wilaya ya Kusini Unguja Kibibi Mwinyi akizungumza na Wananchi wa Paje kuhusu kutoa mashirikiano kwa Madaktari wa Shirika la utoaji wa Miwani la Sweden wakati akizindua huduma za macho huko Kituo cha Afya Paje Mkoa wa Kusini Unguja.

Mkuu wa Kitengo kutoka Shirika la utoaji Miwani la Sweden Caroline Schiller akifanya zoezi la kumpima Macho Mtoto Kassim Juma katika Kituo cha Afya Paje.
Mmoja kati ya Wananchi waliyojitokeza kupata huduma za macho Maua Sleiman Said akijaribu kusoma wakati akipatiwa huduma hiyo na Daktari kutoka Shirika la utoaji wa miwani la Sweden Julia Sandberg katika Kituo cha Afya Paje Wilaya ya Kusini.
Baadhi ya Wananchi waliofika kupata huduma za macho huko kituo cha Afya Paje Mkoa wa Kusini Unguja.

 

Loading