Uzinduzi wa Shahada ya Kwanza kwa Uuguzi na Ukunga

Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dk,Jamala Taib akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Shahada ya kwanza ya Uuguzi na Ukunga  chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA katika Skuli ya Afya  na Sayansi za Tiba hafla iliofanyika katika ukumbi wa Chuo kikuu cha Taifa Suza kampasi ya Vuga Zanzibar

Mkurugenzi Mkuu  Wizara ya Afya Dkt Jamala Adam Taib ameutaka Uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA ) kuhakikisha wanapokea wanafunzi wenye sifa  zinastahiki kujiunga na Chuo hicho  jambo ambalo litasaidia kutoa wahitimu wenye kiwango bora  .

 Akiyasema hayo huko katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar  (SUZA), Vuga, wakati wa Uzinduzi wa Shahada ya Kwanza kwa Uuguzi na Ukunga.

Alisema wanafunzi ambao wanasifa kulingana na kiwango chao cha ufaulu ndio wanaostahiki kujiunga na chuo katika kada ya uuguzi na ukunga  kwa lengo la kupata ufaulu wenye hadi na kiwango bora .

Alisema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein aliunganisha vyuo mbali mbali ikiwemo chuo cha afya kwenda Chuo cha Taifa kwa lengo lakuleta msukumo wa kuzipandisha hadhi kada mbali mbali ili kuweza kufikia malengo ya kitaaluma .

Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi na Wakunga (Sssociate Dean wa Skuli ya Afya na SAYANSI ZA Tiba(SUZA)Amina Abdulkadir akitoa historia ya uuguzi na Ukunga Zanzibar katika Uzinduzi wa Shahada ya kwanza ya Uuguzi na Ukunga chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA katika Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba hafla iliofanyika katika ukumbi wa Chuo kikuu cha Taifa Suza kampasi ya Vuga Zanzibar.

Nae Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Amina Abdukadir Ali amewataka waunguzi na wakunga  kuwa imara katika kutekeleza majukumu yao kwa kuwasaidia wananchi.

“Mfanyekazi  kwa kuwahudumia wananchi kuimarisha hadhi na ubora  kiafya muhakikishe hakuna mtu anaeachwa nyuma kupatiwa huduma za afya ikiwemo mama na watoto sio wakati wa masihara ni wakati wa kuleta mabadiliko.  “alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha aliwataka Wauguzi na Wakunga kuwa na  tabia nzuri ya kunyenyekea wagonjwa kwa kufuata maadili na sheria za  kazi  ili wasiingie katik matatizo .

Kwa Upande wa Naibu Makamo Mkuu wa Chuo cha Taifa (SUZA) Dk Haroun Maalim aliwapongeza wanafunzi kwa kujiunga katika fani ya uuguzi na ukunga fani ambayo hapo awali ilikuwa ikizaraulika .

Alisema hadi sasa wamepokea jumla ya wanafunzi 29 kwa awamu  ya mwanzo ya Shahada ya Kwanza kwa Uuguzi na Ukunga ambao wanatarajia kuanza masomo  yao .

Nae Mrajisi wa Baraza la Wauguzi  Vuai Kombo Haji amesema fani ya uunguzi na ukunga ni ya muda mrefu kwa upande wa Zanzibar imeanza katika mwaka 1938 hadi sasa, ulianzia katika ngazi ya cheti , stashahada hadi  sasa inaanzishwa Shahada ya Kwanza  ya uuguzi na ukunga .

Fani ya uuguzi na ukunga ifikapo 2020 itaadhimisha kutimiza miaka 200 katika kada ya uuguzi na ukunga duniani

Loading