WAFANYAKAZI WA BOHARI KUU YA DAWA ZANZIBAR WAPATIWA MAFUNZO YA LUGHA YA ALAMA.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Asha Ali Abdulla akitoa hotuba ya uzinduzi  wa Mafunzo ya Lugha ya alama kwa wafanyakazi wa Bohari kuu ya dawa  katika Ukumbi wa Bohari kuu ya Dawa Maruhubi Zanzibar

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Asha Ali Abdalla amempongeza  Mkurugenzi Bohari kuu ya Dawa Zahran Ali Hamad kwa kutekeleza kwa vitendo mafunzo ya lugha ya alama kwa wafanyakazi wake .

Amesema utekelezaji wa mafunzo ya lugha ya alama ni jambo muhimu sana ambalo litasaidia kuondoa changamoto zinazowakabili wananchi wenye mahitaji maalum kuweza kufahamiana kwa urahisi pale wanapo taka kupatiwa huduma .

Hayo ameyasema huko katika Ukumbi wa Bohari kuu ya Dawa Maruhubi Zanzibar,.alipokuwa akifungua mafunzo ya lugha ya alama kwa wafanyakazi wa Bohari hiyo.

Alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa Taasisi  zote ambazo zinatowa huduma kwa wananchi ili kuweza  kujenga uelewa kwa wananchi wenye mahitaji maalumu hasa visiwi kwa kupata huduma kama wengine.

“Sera ya Afya tutoe huduma ya afya bila ya ubaguzi kwa watu wote hata kama wanamahitaji maalumu ya viungo,akili wasioona viziwi na wenye maradhi ya ngozi  wote wana haki sawa katika kupata huduma “alisema Katibu huyo .

Katibu huyo amewataka wenye kutoa huduma pamoja na jamii kiujumla  ibadilike  kwa kujuwa tofauti zilizopo baina yao  na kuhakikisha nao wanapatiwa huduma kwa kuzingatia wao hawako katika mfumo wa kawaida kutokana na mapungufu walionayo.

Mkurugenzi Bohari kuu ya Dawa Zahran Ali Hamad akitoa hotuba kwa wafanyakazi wa Bohari kuu katika hafla ya Uzinduzi wa Mafunzo ya Lugha ya alama kwa wafanyakazi hao yanayofanyika katika Ukumbi wa Bohari kuu ya Dawa Maruhubi Zanzibar

Nae Mkurugenzi Bohari kuu ya Dawa Zahran Ali Hamad aliwataka wafanyakazi hao kuwa makini katika kujifunza mafunzo wa kuweza  kujenga uelewa wa kuimarisha mawasiliano wakati wanapotoa huduma kwa wananchi hao ili kuwaondoshea changamoto wanazokumbana nazo .

Aidha alisema ni jambo la kusikitisha kuona watoaji wa huduma za afya ikiwemo madaktari  kutoelewana na mgonjwa mwenye mahitaji maalumu  jambo ambalo linachangia unyanyasaji na kuhisiwa wanapoteza muda kwa kutofahamiana kwao .

Jambo hilo linachangia kupata unyonge kwa kushindwa kujielezea na kutolewa ukali,  kukosa uelewa wa matumizi ya dawa wanazopewa pia kukaa foleni kwa muda mrefu kutokana na kutosikia wakati wakiitwa kupatiwa huduma.

Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi Wizara ya Afya Ramadhan Khamis akitoa nasaha kwa wafanyakazi wa Bohari kuu katika hafla ya Uzinduzi wa Mafunzo ya Lugha ya alama kwa wafanyakazi hao yanayofanyika katika Ukumbi wa Bohari kuu ya Dawa Maruhubi Zanzibar

Kwa upande wa Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi Wizara ya Afya Ramadhan Khamis alisema  uanzishwaji wa mafunzo hayo muhimu kwa watoa huduma itasaidia kuonyesha njia kwa Taasisi mbali mbali kujifunza ili kusaidia watu wenye mahitaji maalum.

Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Zanzibar(CHAVIZA)Bi Asha Ali akitoa hotuba katika hafla ya Uzinduzi wa Mafunzo ya Lugha ya alama kwa wafanyakazi hao yanayofanyika katika Ukumbi wa Bohari kuu ya Dawa Maruhubi Zanzibar

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Zanzibar (CHAVIZA) Asha Ali  amesema amefurahishwa kwa juhudi ya Wizara ya Afya kuanzisha mafunzo ya alama za vidole kwa watendaji wake ili kuweza kuwarahisishia mawasiliano pale wanahitaji  huduma .

Mafunzo hayo ni ya muda mrefu ambayo yamewashirikisha wafanyakazi wote wa bohari kuu  ya madawa kwa kila siku nne za masaa mawili ya mwisho katika saa za kazi .

Loading