MAFUNZO KWA WAFAMASIA

Mfamasia Mkuu wa Serikali  Habibu Ali Sharifu  amewataka wafamasia kuwa  waaminifu katika utendeji  wa kazi zao ili kutekeleza maadili ya kazi  kufanya hivyo kutaisaidia azma ya Serikali kuhakikisha wananchi wanapatiwa matibabu bure .

Hayo ameyasema huko katika ukumbi wa Shekhe Idrisa Abdulwakili,kikwajuni wakati wa mafunzo  kwa wafamasia wa  Zanzibar amesema si mwema wafamasia kukosa uwadilifu katika kazi zao ..

Alisema wengi wa Wafamasia hukosa  uwaaminifu kwa kuhitaji utajiri wa haraka haraka jambo ambalo linachangia kufikia lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwapatia huduma za tiba na dawa wananchi wake .

Aidha alisema Serikali inaweka bajeti kubwa ya ununuzi wa dawa kwa lengo la kuwasaidia wananchi wanyonge ambao wanasumbuliwa na maradhi mbali mbali lakini watendaji wa kazi ambao wameaminiwa hujitoa uwaminifu na kufanya ubadhilifu .

Nae Mkufunzi kutoka Bohari Kuu ya Madawa Saidi  Yussuf amesema tayari mfumo mzuri umeshawekwa wa kuweza kudhibiti ubadhilifu unaofanywa katika vituo mbali mbali vya afya.

Alifahamisha katika usimamizi wa  dawa hizo Idara ya Bohari inapokea inahifadhi pamoja na kusambaza katika vituo vya afya chini ya usimamizi wa Mfamasia Mkuu wa Serikali .

Aidha alisema iko haja ya kufanya ukaguzi katika vituo kwani tabia iliyozoeleka kwamba wafamasia wanaweka mlimbikizo wa dawa ambazo mahitaji yake hayapo katika kituo na kushindwa kutoa taarifa ambayo itasaidia kutumika katika vituo vyengine .

Hata hivyo alisema ukaguzi umegudua kwamba kuna baadhi ya maduka ya madawa kuweka dawa zilizomaliza muda wake na dawa ambazo ziko katika muda kufanya hivyo ni kinyume na taratibu, dawa zilizomaliza muda lazima zitengwe sehemu maalum .

Kwa upande wa mamlaka ya kuzuiya rushwa na uhujumu uchumi Abubakar Mohamed amesema kuwa madhumuni ni kukabili tatizo la matumizi mabaya ya mali na mapato katika sehemu zote za kazi .

Alieleza kuwa kutoa mafunzo ya  rushwa na ubadhilifu wa mali za serikali kwa  Wafamasia kutawasaidia kukuza uelewa wa athari mbali mbali za rushwa zinazotokana na usimamizi dhaifu wa majukumu ya kazi zao ambayo inachangia kupoteza haki zao na kuwasababishia matatizo familia zao.

Alieleza makosa ya rushwa na kuhujumu uchumi katika uwakala kifungu cha 36 cha sheria N0, 1 ya mwaka 2012 mtu atakuwa amefanya kosa ikiwa kwa njia ya rushwa amepokea ametoa ameahidi au ameshawishi au kuonyesha upendeleo .

Amewataka wafamasia wakitoa dawa kurikodi hadi namba za simu za mgonjwa ili kuweza kuhakikisha dawa zinatumika kwa mujibu ya matakwa ya serikali ilivyopanga na kuweza kuudhibiti ubadhilifu wa mali za serikali .

Aidha alisema kuwa Serikali itahakikisha wale watendaji wanaoutumia mwanya kwa kufanya vitendo vya ubadhilifu wa mali kwa njia moja au nyengine itaendelea kuwadhibiti kwa kutumia vifaa vilivyowekwa pamoja na kuiunga mkono serikali ya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma ya matibabu bure

Loading