WIZARA YA AFYA YATILIANA SAINI MKATABA WA UNUNUZI WA DAWA NA BOHARI KUU YA DAWA MSD ZANZIBAR

Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dk Jamala Taibu kulia akitiliana saini na Meneja wa Kanda ya Dare-es-Salaam Bohari kuu ya Dawa MSD Celestine Haule  mkataba wa makubaliano wa Ununuzi wa Dawa baina ya Wizara ya Afya na Bohari kuu ya Dawa MSD hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.

Wizara ya Afya Zanzibar imetiliana saini hati ya makabdihiano ya ununuzi wa madawa kati ya Bohari ya dawa  Tanzania Bara na Zanzibar   kwa lengo la kuimarisha huduma za afya nchini .

Utiaji saini huo ulifanywa na Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Jamala Talib na Meneja wa Kanda ya Dare-es-Salaam Bohari kuu ya Dawa MSD  Celestine Haule ambao ulifanyika huko Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar .

Utiaji saini huo ni wa muda wa miaka mitatu wenye lengo la kutoa huduma kwa kiwango kinachohitajika katika kuboresha usafirishaji wa dawa na ununuzi  kutoka kiwandani.

Nae Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohammed amesema kuwa ni busara kutumia huduma za ndani ya Tanzania kwa kurahisisha upatikanaji wa dawa kwa urahisi.

Aidha alisema kuwa katika utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi Zanzibar ni kuhakisha wananchi wanapatiwa huduma za matibabu bure na kuona mashirikiano yanaimarika katika utoaji wa huduma.

Vilevile alisema idadi imeongezeka ya wagonjwa kwa kuwepo ongezeko la wagonjwa ambao wanahitaji huduma ya tiba na dawa hivyo Serikali imeongeza idadi ya madaktari ili kuweza kutoa huduma.

Hata hivyo alisema kuwa msimamo wa Serikali katika kuimarisha huduma zake imepanga kununua dawa viwandani na sio kwa watu binafsi ili kuona dawa zinakuwa na kiwango kinachohitajika.

Loading